Ads

Uingereza yatwaa Kombe la Dunia la Vijana U-20...


 Mshambuliaji Dominic Calert-Lewin ameiongoza England kutwaa ubingwa wa U-20 kwenye Kombe la Dunia la vijana leo Jumapili, baada ya kuifungia timu yake bao katika kipindi cha kwanza.
Mwaka 1966 ndio ilikuwa mara ya mwisho kwa Waingereza kucheza fainali kubwa ya dunia ikiwa ni miaka 51 iliyopita waliposhinda Kombe la Dunia.
Ushindi wa vijana hao, ni faraja kwao kutokana na matokeo yasiyoridhisha ya timu yao ya wakubwa kwenye mashindano mbalimbali ambayo huishia njiani.
Shukrani kwa mlinda mlango wa Uingereza Freddie Woodmans ambaye aliokoa mkwaju wa penati kipindi cha pili.
Golikipa wa Uingereza alikuwa nyota wa mchezo huo kwani Venezuela walimuandama sana kwa mashambuli na shuti la mshambuliaji wao Lucena liligonga mwamba shambulizi ambalo lilikuwa hatari zaidi kwa Waingereza.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.