Ads

Nahodha wa stand afunguka mazito...


Image result for stand united

 Nahodha wa Stand United, Jacob Masawe amesema hataweza kusaini mkataba mpya wa kuichezea timu hiyo kama itashindwa kumlipa fedha yake ya usajili wa msimu uliopita pamoja na mishahara yake ya miezi minne.
Masawe ambaye ameitumikia Stand United kwa miaka miwili sasa, alisema kuwa kuendelea kuitumikia timu hiyo bila malipo hayo ni utumwa na kutokuwa na utimamu wa akili.
Alisema kuwa anaamini kwamba muda ukifika kama hatamalizana na uongozi wa klabu hiyo basi atafuata taratibu za kisheria za kudai stahiki zake, huku akiendelea kufanya mchakato mwingine kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu.
"Viongozi wametueleza kuwa watatulipa haki zetu na kwamba haki zetu hazitapotea, ila siwezi kusaini mkataba mwingine bila malipo hayo kulipwa, wanilipe kwanza ndipo tuanze biashara nyingine, kiukweli sitakuwa tayari kuendelea kuwepo hapa kama hawatatimiza ahadi yao," alisema.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.