Ads

Arsenal, mbona mtamuelewa tu Wenger....


Image result for alexander golovin

London, England. Arsenal imekamilisha usajjili wake wa pili katika msimu wa kiangazi kwa kumsajili kiungo kutoka klabu ya CSKA Moscow, Alexsandra Golovin ambaye atahamia kwenye dimba la Emirates.
Gazeti la Mirror liliripoti kwamba tayari klabu hiyo imetenga Pauni 10 milioni kwa ajili ya klabu hiyo ya Urusi na uhamisho utakamilika hivi karibuni.
Mchezaji huyo mwenye miaka 21 amekuwa akichezea CSKA tangu mwaka jana na ameiwezesha timu hiyo kumaliza katika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu nchini humo wakiwa nyuma ya Spartak Moscow.
Golovin amefanikiwa kufunga mabao manne na kutoa pasi 20 za mabao, huku uwezo wake ukionekana kuimarika jambo ambalo Arsenal wanaamini atakisaidia kikosi hicho simu ujao.
Awali, mchezaji huyo alikuwa akiwindwa na mabigwa wa England, Chelsea.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.