Ads

Jean Cloud agombaniwa na Simba na yanga...



Dar es Salaam. Kiungo Iranzi Jean-Claude aliyekuwa anakipiga katika klabu ya APR ya nchini Rwanda amegeuka kuwa lulu, baada ya kugombaniwa na vilabu vya Simba na Yanga.
Kiungo huyo pia alifanikiwa kukipiga katika klabu ya Mvk ya Slovakia baada ya kuondoka APR lakini alipokuwa nchini humo alipata matatizo ya kifamilia na kumfanya avunje mkataba na klabu hiyo.
Meneja wa mchezaji huyo, Gakumba Patrick alisema Tanzania ni vilabu viwili Yanga na Simba, vimeonyesha kuhitaji huduma ya mchezaji huyo ila Kenya nao wameshtukia dili hilo na hivyo ataangalia wapi penye maslahi mazuri.
"Kijana alikuwa anapenda aje acheze Tanzania lakini Tusker ya Kenya nao wameniambia wanamtaka tunaenda katika mazungumzo kuwasikiliza kuona inakuaje, lakini kikubwa maslahi tutaangalia ofa yao," alisema.
Hata hivyo nahodha huyo wa zamani wa timu ya Taifa na Rwanda na klabu ya APR anatakiwa na klabu ya Saint George ya nchini Ethiopia.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.