maneno ya Miraji Adam baada ya kuanguka saini...
Dar es Salaam. Beki Miraj Adam aliyekuwa anakipiga katika klabu ya Africa Lyon iliyoshuka daraja, amejiunga rasmi na klabu ya Singida United kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu.
Adam alisema, "Nimekuja mjini leo asubuhi baada ya jana kutumiwa mkataba wangu, nimeusoma na kuuelewa nimeona kuwa wapo makini katika masuala ya mpira ndio maana nimeamua kujiunga nao," alisema.
Miraj alitokea katika klabu ya vijana ya Simba na kulelewa mpaka kupandishwa katika kikosi cha wakubwa, lakini baadaye walimtoa kwa mkopo Coastal Union na alionyesha kiwango kizuri ambacho kiliwashawishi Lyon kumsajili.
Miraj alithibitisha kuwa ni kweli alitumiwa mkataba na uongozi wa klabu hiyo na baada kuupitia na mwanasheria wake, ameona bora amwage wino katika timu hiyo.
Aliongeza kwa kusema kuwa anajua kuwa klabu hiyo imejipanga kuleta ushindani katika msimu ujao hivyo atahakikisha anajitunza ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chake kipya.
No comments