Mbeya city mtu tatu ndani...
Dar es Salam. Klabu ya Mbeya City imefanikiwa kuwasajili nyota wa tatu kwa mpigo katika kujiimarisha na msimu ujao wa Ligi Kuu ambao unatarajiwa kuwa na msisimko wa aina yake.
Mbeya City imefanya usajili wake wa kimya kimya jijini Dar es Salaam kwa kuwasajili mabeki Erick Kiyaruzi aliyekuwa amefungiwa na Kagera Sugar, Ally Lundenga kutoka Mtibwa Sugar na Ramadhani Malima kutoka Toto Africans.
Beki mpya wa timu hiyo Ally Lundenga amesema licha ya kwamba alikuwa Mtibwa kwa muda mrefu, ameamua kuondoka kikosini hapo kwa ajili ya kutafuta changamoto mpya.
No comments