Ads

Luizio huenda akaachwa na Simba..,


Image result for liuzio wa simba

Dar es Salaam. Simba ipo kimya kuhusiana na mchezaji Juma Luizio ambaye anamaliza mkataba wake na Zesco Julai mwaka huu, ameamua kusoma alama za nyakati na kutamka kuwa anaweza kurejea Zambia.
"Viongozi wa Zambia ndiyo ambao wameniambia tutafanya mazungumzo ya mkataba mpya, lakini kwa sasa bado nipo mapumziko na mambo yakiwa sawa nitaweka wazi nitacheza wapi," anasema.
Luizio anasema usajili wa Simba, katika nafasi yake haumuumizi kichwa kwani anaamini anaweza kucheza zaidi ya nafasi nne pale mbele.
"Nina uwezo wa kucheza nafasi nne za mbele kwa hiyo usajili wao haunisumbui kwamba kama walikuwa wananihitaji nitakuwa sina pa kucheza si kweli," anasema

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.