Ads

Tetesi za usajili, Mbappe karibuni kutua PSG...


Image result for mbappe

Paris Saint Germain imepiga hatua kubwa katika kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa Monaco, Kylian Mbappe.
Kwa mujibu wa gazeti la L’Equipe, mkurungezi wa ufundi wa PSG, Antero Henrique amekuwa na mawasiliano na wakala wa mchezaji huyo.
Henrique anaonekana amepiga hatua kubwa baada ya kubainisha kuwa anategemea kumsajili mchezaji mwenye jina kubwa anayecheza  Ligue 1.
Inaaminika mahusiano mazuri kati ya Monaco na PSG itafanikisha usajili huo kwa wepesi zaidi katika siku za karibuni.
Chelsea hivi karibuni iliingia katika mbio za kumwania mshambuliaji huyo mwenye miaka 18, ambaye pia anatajwa kutakiwa na Arsenal na Manchester United.
L’Equipe pia, lilidai kuwa Arsenal ilikuwa tayari kutoa pauni 87milioni kwa ajili ya nyota huyo, lakini Monaco imekataa.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.