Ads

Liverpool mbioni kumnasa Mbappe....


Image result for mbappe


London, England. Liverpool imeingia katika mbio za kumwania chipukizi wa Monaco, Kylian Mbappe, 18, ingawa imeelezwa kwamba PSG ipo katika nafasi nzuri za kumtwaa kinda huyo wa Timu ya Taifa ya Ufaransa aliyetemba msimu uliopita.
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp imedaiwa kuwa ameongea na wawakilishi wa staa huyo kwa ajili ya kumshawishi atue Anfield ingawa pia PSG nayo imeongea na wawakilishi hao hao huku ikionekana kueleweka zaidi.
Mbappe ambaye alitamba katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya akiifikisha Monaco nusu fainali huku pia akiipa ubingwa wa Ufaransa amekuwa akitazamwa kwa karibu pia na klabu za Real Madrid na Arsenal.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.