Man United yatumia mabilioni kusajili mabeki...
Uhamisho wa Victor Lindelof kutoka Benfica kwenda Manchester United imeifanya klabu hiyo ya England kuweka rekodi ya kutumia euro 161 milioni katika kununua mabeki katika misimu minne iliyopita.
Daley Blind, Luke Shaw na Marcos Rojo wote wamesajili miaka mitatu iliyopita chini ya kocha Louis van Gaal, kabla ya Matteo Darmian na Eric Bailly kutua Old Trafford kati ya mwaka 2015 na 2016.
Hiyo ni ishara kwamba Man United ina wastani wa kununua beki moja katika misimu minne iliyopita.
Mchezaji aliyesajiliwa kwa gharama kubwa hivi karibuni Bailly, japokuwa beki huyo tangu ametua Villarreal mwaka jana amekuwana mchango mkubwa kwa Manchester United.
Gharama za usajili wa mabeki Man United
2017/18. VĂctor Lindelof (Benfica, 30m euros, siyo rasmini)
2016/17. Eric Bailly (Villarreal, 38m euros)
2015/16. Matteo Darmian (Torino, 18m euros)
2014/15. Marcos Rojo (Sporting CP, 20m euros)
2014/15. Luke Shaw (Southampton, 37.5m euros)
2014/15. Daley Blind (Ajax, 17.5m euros)
No comments