Ads

Man United yamng’oa beki wa Benfica...


London, England. Manchester United imethibitisha imefikia kufikia makubaliano na Benfica ya kumsajili beki, Victor Lindelof kwa Pauni 40 milioni pamoja na kumpa marupurupu mengine.
Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo ilisomeka, “Manchester United inapenda kuwatangazia kwamba  imefikia makubalianao na Benfica kuhusu kumsajili Victor Lindrlof.  Pia baada ya kukamilisha uchunguzi wa kitabibu pamoja na  na uhamisho wa kimataifa na masuala yake binafsi taarifa zaidi zitatolewa.”
Kusajiliwa mchezaji huyo kumehitimisha taarifa za kuhamia klabuni hapo zilizoenea tangu dirisha la usajili mwezi Januari.
Hata hivyo, Kocha Jose Mourinho aliamua kuzima mipango hiyo akisema hakuwa tayari kumchukua mchezaji mwingine katitakati ya msimu.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.