Ads

Bufffon anahitaji mrithi wake mapemaaa....

Image result for buffon

Italia. Kipa wa Juventus, Gianluigi Buffon ameitaka klabu yake kulipa kipaumbele suala la kumsajili nyota wa AC Milan kwa kuwa anatarajia kustaafu soka muda siyo mrefu.
Buffon ambaye mkataba wake unamalizika mwka 2018, amewaambia uongozi wa kalbu hiyo kumwandaa mrithi wake kabla ya kufika wakati wa kustaafu.
Kipa huyo aliyekosa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu wakati timu yake ilipokutanana Reala Madrid, ameibuka kuwa miongoni mwa makipa bora baada ya kuiwezesha timu hiyo kufika fainali.
Licha ya Buffon kupendekeza timu hiyo kuangalia uwezekano wa kumchukua kipa kijana Bonnarumma, pia mwingine aliyemtaja ni kutoka Arsenal, Wojciech Szczesny ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na mabingwa hao wa Seria A.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.