Ads

Taifa stars kujipanga tena...



Image result for taifa stars

KOCHA wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Salum Mayanga amesema baada ya kupata sare ya bao 1-1, dhidi ya Lesotho katika mchezo wa kufuzu Mashindano ya Mataifa Afrika mwakani ambayo yatafanyika nchini Cameroon mwaka 2019, wanatakiwa kusahau matokeo hayo ila wanatakiwa kujipanga na kupata ushindi katika mchezo ujao.
Bao la Taifa Stars lilifungwa na nahodha Mbwana Samatta katika dakika ya 27, kipindi cha kwanza kabla ya kusawazishwa na Thapelo Tale dakika  ya 34, ambaye alishindwa kuendelea na mchezo baada kuumia.
"Tunachotakiwa ni kusahau yaliyotokea katika mchezo huu na kuanza kujipanga na kufikilia mechi ijayo dhidi ya Uganda ambayo tutacheza hapa hapa nyumbani ili kupata ushindi na kujiweka katika wakati mzuri wa kuweza kufuzu katika michuano hiyo," alisema.
"Tulikuwa na mipango ya kupata ushindi lakini wapinzani baada ya kusawazisha walirudi nyuma wote na kuzuia tangu hapo jambo ambalo lilituwia vigumu na kushindwa kupenya ngome yao na mechi kumalizika hivyo," alisema Mayanga ambaye ni kocha wa muda wa kikosi cha Stars.
Taifa Stars wapo katika kundi L  na timu za Cape Vade, Uganda na Lesotho ambao waliwashangaza Stars kwa kutoka nao sare kwani walikuwa wakionekana kama vibonde katika kundi hilo.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.