Ads

NILIKWEPA Mawe Manne Kabla ya Kuchomwa Mkuki Mdomoni’-Augustine Mtitu



Moja ya tukio lililomake headline wiki hii ni kuhusu mkulima, Augustino Mtitu aliyechomwa mkuki mdomoni na ukatokea shingoni kwa kile kilichoelezwa ni mgogoro wa wakulima na wafugaji huko kijiji cha Dodoma Isanga kata ya Manzese wilaya ya Kilosa Mororgoro.

Ameongea haya:

‘Kuna wafugaji waliingiza ng’ombe kwenye shamba la jirani, kijana mmoja akatoka wakamchapa fimbo, nilipoenda kusaidia wakaanza kunishambulia kwa mawe, nikakwepa mawe manne na nilipotaka kugeuka nikimbie nikashtukia mkuki umenichoma mdomoni’;-Augustino Mtitu

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.