Mwalimu mkuu wa shule alikopigwa mwanafunzi Tz asimamishwa kazi..........
Serikali ya Tanzania imeagiza kufanyika kwa uchunguzi kuhusu kanda ya video ilioonyesha kundi moja la walimu likimpiga mwanafunzi.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo tayari amesimamishwa kazi kwa mda kwa kutochukua hatua hata baada ya kugundua kuhusu kisa hicho ,taarifa ya serikali imesema.
Raia wa Tanzania katika mitandao ya kijamii walionyesha hasira zao ,wakiitaka serikali kuchukua hatua dhidi ya washambuliaji hao.
Video hiyo ambayo haijakaguliwa inaonyesha mwanafunzi mmoja akipigwa na kundi la walimu katika kile kinachoonekana kuwa chumba cha wafanyikazi wa shule.
Katika kanda hiyo ya sekunde 38,takriban watu watano wanaonekana wakikabiliana na kushambulia mvulana huyo aliyeanguka chini kwa kumpiga ngumi pamoja na mateke.
Adhabu ya kupigwa viboko ni haramu nchini Tanzania,na kisa hicho cha hivi karibuni kinatarajiwa kuzua mjadala kuhusu utekelezwaji wa sheria hiyo katika shule za taifa hilo.
No comments