Ads

Mzee wa miaka 114 atoa siri ya kuwa na maisha marefu.......

 Ingawa anaonekana mdogo wa umri, mwanamume huyu ana miaka 114.

Kwa kumwangalia tu Bernardo Lapallo, huwezi kusema kuwa ana miaka 114.

Kulingana na mwanamume huyo, ni vyema kuutunza mwili wako ili kuwa na maisha marefu.
Mzee huyo amesema kuwa husoma kila siku na kufanyisha kazi ubongo wake kwa kusuluhisha changamoto za maneno na hukimbia kila siku kilomita 2.5.

Uso wake Bernardo hauna mikunjo kama unavyotarajia kwa mzee wa umri wake.

Mzee huyo alisema huwa hula mboga kwa wingi na hunywa maji safi, na mengi kila siku.

Mwanamume huyo alieleza kuwa kitunguu saumu, mdalasini, mzeituni na asali husaidia sana mtu kuwa na afya njema na kusalia mchanga

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.