Ads

YANGA YAPATA PIGO, KIPA WAKE NAMBA MOJA DEO MUNISHI AFIWA NA BABA YAKE.......


1Mlinda lango namba moja wa Yanga Deogratius Munishi ‘Dida’ amefiwa na baba yake mzazi leo mchana, imeelezwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa kwenye ukurasa wa Facebook wa Naipenda Yanga bado chanzo cha kifo cha baba mzazi wa kipa huyo hakijawekwa wazi

Taarifa hiyo inaeleza hivi: “TANZIA…Uongozi wa yanga unasikitika kutangaza kifo cha baba yake na mlinda mlango wetu deogratius munishi ‘Dida’. Baba yake na dida amefariki leo mchana! Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi! Msiba utakua mikoroshini.Pumzika kwa amani mzee wetu. POLE SANA DEO MUNISHI ‘Dida’.”

Hata hivyo katika mchezo wa leo Dida amecheza kwa umahiri mkubwa na kuisaidia timu yake kupata clean sheet.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.