Ads

WAKULIMA wa mazao ya biashara Iringa wameziomba taasisi za kibenki kuangalia namna ya kuboresha njia za utoaji mikopo............


WAKULIMA wa mazao ya biashara mkoani Iringa ameziomba taasisi za kibenki nchini kuangalia namna ya kuboresha njia za utoaji mikopo kwa wateja wao na hasa wale walio katika sekta ya kilimo kwa lengo la kufanikisha wakulima wengi kupata mikopo hiyo.

Wakulima ambao wengi wao ni sehemu ya wana hisa wa benki ya MUCOBA wametoa ombi hilo ktk mkutano mkuu wa 17 wa wana hisa wa benki hiyo na kuongeza kuwa sasa hali ya upatikanaji wa mikopo si nzuri sana na hasa ukizingatia kilimo ni biashara inayotegemea sana hali ya soko.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa benki ya MUCOBA Bw. Ben Mahenge anasema wakulima wanapaswa kubadili namna ya uendeshaji wa kilimo chao ili kuepuka kupata hasara endapo hali ya kilimo haitakuwa kama walivyotarajia.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.