Ads

Fabregas amkana Conte

Cesc Fabregas Kiungo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas amepinga madai kwamba alikosana na meneja wa klabu hiyo Antonio Conte. Meneja huyo aliripotiwa kumtaka mchezaji huyo wa miaka 29 kuondoka kabla ya kukamilika kwa siku ya mwisho ya uhamisho. Fabregas hatahivyo amechapisha katika mitandao ya kijamii akisema kuwa wawili hao wana uhusiano mzuri na kwamba ataendelea kuichezea Chelsea. Image Mkufunzi wa Chelsea Conte ''Mbali na ilivyoandikwa, mkufunzi Conte hajawahi kuniambia kwamba niondoke '',aliandika Fabregas. ''Aliniambia kwamba ananitegemea na mimi namtegemea.Nitaendelea kuichezea klabu hii hadi mwisho na iwapo nitahitajika nitajitolea''.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.