DAAA! KWELI HATA OMONG KAKUBALI TSHISHIMBI NISHIIIDAA!
HAIKUWA kazi rahisi, hiyo ni kauli ya Kocha Mkuu wa Simba Mcameroon, Joseph Omog, ambaye timu yake ilifanikiwa kunyakuwa ubingwa wa Ngao ya Jamii juzi kwa kuwafunga mahasimu wao Yanga penalti 5-4 huku akimtaja kiungo Papy Tshishimbi alikuwa kikwazo kwa nyota wake.
Omog aliliambia gazeti la Nipashe kiungo huyo wa kimataifa wa Yanga kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuwa alionyesha kiwango cha juu katika mchezo huo na ndiye alikuwa kikwazo kwa wachezaji wake kwenye mchezo huo ambao dakika 90 za kawaida zilimalizika kwa sare ya bila kufungana.
Kocha huyo alisema: "Tumemuona, tunajipanga, ila ni wazi kuwa timu zote zilicheza kwa tahadhari lakini nasikitika washambuliaji wangu walishindwa kufunga ndani ya dakika 90, walipoteza nafasi za kufunga walizotengeneza."
"Ulikuwa mchezo mgumu sana, lakini nashukuru Mungu tumeibuka washindi, akili yetu sasa tunaielekeza kwenye Ligi Kuu ambayo tunaanza na Ruvu Shooting, hautakuwa mchezo mwepesi kwa sababu nao pia wamepata nafasi nzuri ya kutusoma," alisema Omog.
Kocha huyo alimtaja mchezaji mwingine wa mabingwa wa Ligi Kuu Bara ambaye alichelewesha furaha ya ubingwa wao kuwa ni Thabani Kamusoko, ambaye juzi alisimama kama nahodha wa Yanga.
"Tshishimbi ni mzuri, na Kamusoko pia alitusumbua, tutajipanga vizuri kuwakabili katika mechi ya ligi tutakapokutana, kwa upande wangu vijana walifanya vizuri na kama nilivyosema mechi ilikuwa ni ngumu kama tulivyoitarajia," Omog aliongeza.
Kiungo mpya wa Simba Mnyarwanda Haruna Niyonzima alisema anafurahi kuanza kwa ushindi dhidi ya Yanga lakini amewataka wachezaji wenzake kujipanga kwa ajili ya ligi kwa kuwa safari ya kukusanya mataji imeanza rasmi.
"Ushindi tuliopata utatusaidia kutufanya tuingie kwenye ligi tukiwa na nguvu, pia kwa sisi wachezaji wapya inatuweka katika nafasi nzuri, tunaahidi kuendelea kupambana kwenye mechi zote zinazofuata," alisema kipa Aishi Manula ambaye kesho wataikaribisha Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Uhuru.
Wakati huo huo kipa Saidi Mohammed anatarajiwa kuondoka nchini wakati wowote kuelekea India kwa ajili ya kutibiwa jeraha la goti ambalo aliumia kwenye mazoezi ya timu hiyo Unguja, Zanzibar.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa kipa huyo aliyeng'ara kwenye michuano ya Cosafa iliyofanyika Afrika Kusini anasubiri kupata visa ya kwenda kwenye matibabu hayo.a
No comments