Ads

KADABLA AAMUA KUZIBA PENGO LA ROONEY UNITED


Manchester United imethibitisha kumrejesha tena mshambuliaji wake ngongoti Zlatan Ibrahimovic ambaye anarejea katika klabu hiyo miezi mitatu tangu alipoondoka katika timu hiyo inayotumia dimba la Old Trafford.


Mshambuliaji huyo raia wa Sweden aliitumikia Man United michezo 46 na kuifungia magoli 28 tangu alipojiunga nayo kwa mkataba huru msimu wa mwaka 2016-17 ikiwa kabla ya kupata majeruhi ya goti, ambayo yalizima ndoto zake za kumaliza msimu huo vizuri.

Taarifa zinaeleza, safari hii Man United watampa jezi namba 10 iliyokuwa ikivaliwa na Wayne Rooney aliyehamia Everton.Hivi karibuni, baada ya kupona, Zlatan alirejea katika viwanja vya mazoezi vya Man United na kuonekana kuwa sasa yuko fiti.

Nguli huyo mwenye miaka 35 alipigwa picha ambayo ikimwonyesha akifanya mazoezi huku akiwa ametiga jezi hiyo namba kumi.

Ibrahimovic, ambaye ameweka rekodi ya kushinda ubingwa katika ligi nne tofauti barani ulaya tangu ajiunge katika soka la kulipwa akitokea klabu ya nyumbani kwao ya Malmo mwaka 1999, amesema amerudi United kukamilisha kazi aliyoianza.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.