Ads

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO IJUMAA AGOSTI 25.2017

Alex Oxlade-ChamberlainHaki miliki ya pichaES

Chelsea wana uhakika wa kumsajili kiungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, 24, kwa pauni milioni 35 kabla ya dirisha la usajili kufungwa Alhamisi ijayo. (Daily Telegraph)
Chelsea wananajaribu kufanikisha usajili wa pauni milioni 15 wa mshambuliaji wa Swansea Fernando Llorente, 32, ambaye alicheza chini ya Antonio Conte, Juventus. (Daily Telegraph)
Juventus wamewasiliana na Chelsea kumuulizia beki wa kati Gary Cahill. (Sun)
Manchester City wamekata tamaa ya kumsajili mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe, 18, kwa pauni milioni 150. (Sun)
Manchester City watapanda dau la tatu la zaidi ya pauni milioni 25 kutaka kumsajili beki wa West Brom Jonny Evans, 29. (Times)
Mchezaji wa Monaco Thomas Lemar amesema angependa zaidi kujiunga na Manchester United badala ya Arsenal. (Duncan Castles)

Chelsea defender Gary CahillHaki miliki ya picha

Zlatan Ibrahimovic amekubali kupunguziwa mshahara wake kwa asilimia hamsini mwezi Januari, baada ya kusaini tena kubakia Old Trafford. (The Sun)
Barcelona wamekubaliana mkataba wa pauni milioni 138 na Borussia Dortmund wa kumsajili mshambuliaji Ousmane Dembele, 20. (L'Equipe)
Barcelona wamesema kiungo Arda Turan, 30, anaruhusiwa kuondoka kwa uhamisho usio na malipo yoyote.. (Sport)
Wakala wa Julian Draxler wa PSG wamekwenda Ujerumani kuzungumza na Bayern Munich kuhusiana na uhamisho wake. (L'Equipe)
Swansea wamepunguza kasi ya kutaka kumsajili kiungo wa West Brom Nacer Chadli, 28, baada ya kuambiwa walipe zaidi ya pauni milioni 25. (Daily Mail)
Crystal Palace wanataka kumsajili kipa wa Tottenham Michel Vorm, 33. (Evening Standard)
Crystal Palace pia wanataka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Munir El Haddadi, 21. (Sport)

Haki miliki ya picha

Winga wa RB Leipzig Oliver Burke, 20, anakaribia kufanya vipimo vya afya kujiunga na West Brom. (Sky Sports)
PSG huenda wakamsajili kipa wa Napoli Pepe Reina. (Talksport)
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii (Kwa Kiingereza) : 

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.