CHADEMA WAFUNGUKA HAYA
Katibu wa Chadema Arusha, Amani Golugwa, amedai wanao ushahidi wa viongozi wa chama hicho wanaorubuniwa kwa rushwa na viongozi wa CCM kwani ni wengi wamekataa ofa hiyo.
Golungwa amesema kuwa kinachofanyika sasa sio siasa, bali rushwa za wazi wazi, hatua aliyodai kuwa haina tija kwa wananchi wala kwa taifa.
"Kama kisingizio ni kumuunga rais mkono, unaweza kufanya hivyo bila kuhama chama, hili tunalizungumza bila kumung’unyamaneno, kwamba hawa viongozi wetu wanaohama wanashawishiwa na pesa na ni wengi wamepewa, wakakataa na ushahidi tunao,"amesema Golugwa .
No comments