BANDA NDO HIVYO TENA KUELEKEA SOUTH.
Beki wa Simba Abdul Banda amekwenda gereza la Keko kuwaaga viongozi wake Evans Aveva na Geofrey Nyange 'Kaburu' kabla ya kujiunga na Baroka FC ya Afrika Kusini.
Banda amesaini mkataba wa miaka mitatu Baroka, lakini kabla hajaondoka kwenda kuanza maisha mapya alikwenda kuwaaga viongozi wake hao waliokuwa rumande kwa tuhuma za kugushi nyaraka za klabu pamoja na kutakatisha pesa.
Banda anaondoka kesho Jumatano kwenda kuanza maisha mapya Sauzi.
Beki huyo aliyekuwa Afrika Kusini na kikosi cha Taifa Stars iliyorejea nchini Jumamosi usiku na asubuhi ya juzi Jumapili ambapo siku hiyo hiyo alikwenda katika gereza hilo kuwaaga viongozi hao na kuomba baraka zao na tayari Simba imeziba nafasi ya Banda kwa kumsajili Salim Bonde wa Mtibwa Sugar.
Meneja wa mchezaji huyo, Abdul Bosnia ambaye aliongozana na mchezaji huyo kwenda Keko, alisema kuwa Banda ni binadamu anaweza kuwa na mapungufu yake na ndiyo maana alipogundua aliamua kuwafuata viongozi wake kuwajulia hali na kuomba baraka zao.
"Kila binadamu ana mapungufu yake, Banda huenda aliwakosea viongozi wa Simba na pengine viongozi nao walimkosea Banda kwa njia moja ama nyingine, hayo mambo yapo katika maisha ya binadamu, hakutaka kuondoka bila kuwaona viongozi wake ambao wamemlea katika kipindi chote hicho na kufanikiwa kupata timu nje," alisema Bosnia.
No comments