Ads

ALICHOKISEMA MMBONDE WA SIMBA MMEKISIKIA ALIKINI?




Beki mpya wa Simba, Salim Mbonde amesema wanaombeza kiwango chake atawaonyesha kwa vitendo uwanjani.
Mashabiki wa Yanga wanawacheka Simba kwa kumsajili beki huyo kutoka Mtibwa Sugar kwamba utakuwa uchochoro mshambuliaji wao, Mzimbabwe Donaldo Ngoma.
Mbonde amesema, aliamua kusaini Simba klabu iliyokuwa imemwania kwa kipindi kirefu kwa sababu aliona ananafasi na amejiandaa vya kutosha na hao Yanga wanaopiga kelele ni fungu la kukosa.
"Nimeshawakaba washambuliaji bora zaidi ya Ngoma na hata huyo Ngoma amebadilika nini kwa sababu kwa kipindi chote alichocheza Mtibwa alikuwa hatambi mbele yake."
"Watu wanapenda nizungumza mimi nitawajibu kwa vitendo, lakini ninachotaka wafahamu, nimesaini Simba baada ya kutafakari mengi nikaona nina nafasi ya kucheza kikosini hapo."
"Simba hawatajutia usajili wangu kikubwa ni ushirikiano tu, hao wanaosema nitakuwa uchochoro wasubiri waone kwa sababu hakuna kipya zaidi ya kubadilisha timu tu, niliokuwa nawadhibiti wakati nipo Mtibwa ndiyo hao hao nitakaocheza nao nitakapokuwa Simba hata huyo Ngoma na wengine,"alisema  Mbonde kwa kujiamini.
Simba itafunga msimu ujao kwa kucheza mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga Agosti19.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.