Ads

Uhusiano wa Namba Hizi na Majini,Shetani ...



Sina kawaida ya kudharau jambo hata kama linaonekana ni la kijinga na nimeshapata faida kubwa kutokana na mtazamo wangu huu,nimeshafanikiwa kwenye mambo mengi ambayo watu waliyaona ni ya kijinga na wengine walijifunza kupitia hili

Leo naomba niwashirikishe jambo hili ambalo ni mewauliza watu kadhaa na wameonekana kunishangaa mtu kama mimi ni kwanini hasa nimeamua kulifuatilia hili,lakini najua kupitia hili naweza kujifunza kitu ambac ho sikua nakijua au nikajikuta napoteza muda wangu,yote haya ni matokeo na nimejiandaa kwa yote

Kuna namba watu wamekuwa wakidai kuwa kama unataka kuzungumza na Shetani au majini basi unaweza kuzipiga,kuna jamaa yangu aliwahi kuzipiga nikiwa nae na simu iliita na ikapokelewa halafu aliulizwa shida yake na alisema lakini aliepokea simu alimuambia kuwa "huwezi wewe na usitusumbue"

Kuna jamaa yangu mwingine alipiga nae simu ilipokelewa na aliambiwa kuwa wapo busy hivyo hawahitaji usumbufu

Ukiangalia namba hizi hazina namba kiunganishi ili ujue hata location ya namba hizi,kitu hiki kimenifanya nijiulize sana kama hii inakubalila kwa mamlaka husika za mawasiliano

Sina ufahamu hasa wa mambo ya mawasiliano na nadhani hapa kuna watu wengi wanaweza kunipa maelezo ya kutosha na nikaridhika kuhusiana na dhana hii kuwa namba hizi ukipiga unazungumza na shetani au majini,sidhani kama jambo hili halina maelezo kwa wale ambao wanajua kuhusu mawasiliano na ndio maana nikaamua kuja kuuliza hapa ili jambo hili niachane nalo

Namba zenyewe ni 11111111111 na 999999999 nadhani zipo na zingine,hebu wakuu nisaidieni hapo ili niweze kujua

Nikwanini hakuna namba kiunganishi lakini simu inaita?
Je ni akina nani wanaopokea simu hizi?

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.