Ads

Rais Sisi aidhinisha kusalimishwa visiwa kwa Saudi Arabia...

File photo taken on 14 January through the window of an airplane shows the islands of Tiran (foreground) and Sanafir (background) in the Red Sea

Haki miliki ya picha
Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi, ameidhinisha mkataba ya umiliki wa visiwa viwili vilivyoko katika maeneo ya bahari ya Sham, kwa Saudi Arabia.
Wakili wa serikali Rafiq Sharif, amesema kuwa amri hiyo ya Rais Sisi, imekuwa sheria na kwa sasa visiwa hivyo vitakuwa ni mali ya Saudi Arabia.
Lakini bado mahakama ya kikatiba inafaa kutoa agizo lake la mwisho, ambapo taasisi hiyo ya kisheria na Bunge la nchi hiyo, ndio yaliyo na uwezo wa kutoa agizo la mwisho.
Egyptians protest in Cairo against the decision to return two Red Sea islands to Saudi Arabia (15 April 2016)Haki miliki ya picha
Muafaka huo, umekuwa ukipingwa na kuzuiwa kufanya kazi katika vuta ni kuvute iliyokuwepo, kwa mwaka mzima nchini Misri.
Hatua ya kuachia Saudi Arabia visiwa hivyo, vilisababisha maandamano na pingamizi kubwa kutoka kwa raia nchini Misri, pale agizo hilo lilipotangazwa mwaka jana na Rais al Sisi.
Mwaandishi wa BBC mjini Cairo, anasema kuwa ikiwa Misri haitokubalia kuachia Saudi Arabia visiwa hivyo, bila shaka huenda wakanyimwa fedha nyingi za uwekezaji kutoka kwa taifa hilo la kiarabu, lenye uchumi mkubwa.
Map
Image captionVisiwa

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.