Ads

Wanamuziki watano wa Hip Hop matajiri zaidi duniani....................

Jay Z


Haki miliki ya picha

Utajiri wa mwanamuziki Jay Z ulipanda kwa asilimia 30 mwaka jana na kufikisha utajiri wake hadi $810m (£626m), kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Lakini kuimarika kwa utajiri wake hakukutosha kumuondoa Sean "Diddy" Combs kutoka kwenye kilele cha wanamuziki matajiri zaidi wa Hip Hop kwa mujibu wa jarida hilo.
Diddy anaongoza akiwa na utajiri wa jumla ya $820m (£633m).
Forbes walisema utajiri wake ulioimarishwa na mikataba ya kibiashara ambayo alitia saini na Diageo kwa ajili ya Ciroc vodka na mavazi yake ya Sean John.

Diddy and CassieHaki miliki ya picha

Lakini rapa na produsa Jay Z alipanda hadi nafasi ya pili sana kutokana na uwekezaji wake wa $200m (£155m) katika kampuni ya kuuza muziki mtandaoni ya Tidal.
Pia, ana mvinyo kwa jina Armand de Brignac, na anamiliki pia Roc Nation.

Diddy and Jay ZHaki miliki ya picha

Mwaka uliopita, utajiri wa Diddy ulikuwa $750m (£579m) na wa Jay Z $610m (£471m).
Forbes waliandaa orodha yao wakizingatia mapato ya miaka ya nyuma pamoja na stakabadhi za kifedha, thamani ya mali inayomilikiwa na wanamuziki hao na pia kwa kuzungumza na wachanganuzi, mawakili, mameneja na wataalamu wengine katika tasnia ya muziki.

Dr DreHaki miliki ya picha

Rapa wa zamani wa NWA Dr Dre kwa sasa ana utajiri wa $740m (£571m) baada ya kuuza Beats kwa Apple mwaka 2014 kwa $3bn (£2.3bn), lakini amepitwa na Jay Z kwa mara ya kwanza.
Baada ya kuuza Beats, alinunua jumba kubwa la kifahari Los Angeles la ukubwa wa futi 14,000 mraba kwa $40m (£31m).
Rapa ambaye pia ni mmiliki mwenza wa Cash Money Records Bryan "Birdman" Williams ana utajiri wa $110m (£85m).

Bryan Haki miliki ya picha

Lebo yake ambayo huimiliki na ndugu yake Ronald (Slim), ina wanamuziki nyota duniani kama vile Drake, Nicki Minaj na Lil Wayne.
Drake utajiri wake unakadiriwa kuwa $90m (£70m).

DrakeHaki miliki ya picha

Aliingia kwenye orodha ya wanahip-hop watano matajiri zaidi duniani na anadaiwa kujizolea jumla ya $1m (£773,000) kila usiku wakati wa ziara yake ya muziki duniani mwaka jana.
Pamoja na kulipwa kutokana an mauzo ya muziki wake, pia ana mikataba ya kibiashara na Apple, Nike na Sprite.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.