ICC kushtaki Wahamiaji haramu wanaopita Libya...............

Mwendesha mashitaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC, Fatou Bensouda amesema timu yake inakusanya ushahidi wa makosa yanayodaiwa kutendwa kwa wahamiaji wanaopitia nchini Libya.
Amesema wahamiaji hao pia wamekuwa wakibakwa kuuawa na kuteswa.
Fatou Bensuda ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba Libya imeonekana kuwa soko la usafirishaji haramu wa binadamu ambapo maelfu ya wahamiaji wasio na msaada, wakiwemo wanawake na watoto wamekuwa wakishikiliwa katika maeneo mbalimbali nchini humo.
Amesema vyanzo vya kuaminika vinaeleza kuwa matukio ya mauaji, ubakaji na utesaji yamekuwa ni matendo ya kawaida katika eneo hilo.
Mahakama hiyo ya ICC inachunguza iwapo makosa hayo yataangukia kwenye makosa yanayohukumiwa na mahakam hiyo.
No comments