Ads

Fakhi wa Kagera Sugar Afunguka ya moyoni........


Hatimaye mchezaji wa Kagera Sugar, Mohamed Fakhi amefuguka ya moyoni na kusema anamshukuru Mungu suala lake limeweza kuisha huku akidai furaha na amani kurejea katika familia yake kutokana na kurudishiwa ushindi wao kutoka kwa timu ya Simba


Fakhi amesema hayo baada kuisha lile vuguvugu la muda mrefu lililokuwa linamuandama kutoka kwa wapinzani wao Simba SC wakidai kuchezeshwa  katika mechi akiwa na kadi tatu za njano na kupelekea kupokwa matokeo yao hapo awali.

"Namshukuru Mungu suala hili limekwisha vizuri....kwa timu yangu kurudushiwa point zake najiona mwenye furaha, amani imerejea familia yangu nayo imetulia kwani suala hili liliwaweka kwenye 'tention' kubwa. Alisema mchezaji huyo

Vile vile Fakhi amewashukuru viongozi wake wa Kagera Sugar pamoja na wachezaji wenzake kwa sapoti waliyokuwa wanampa muda wote huku akisisitizia kuwa nguvu yote sasa anailekeza kwenye michezo yao ya mwisho ya ligi iliyosalia.

Aidha baada ya kurudishiwa matokeo hayo kutoka kwa wanamsimbazi timu ya Kagera Sugar wamekuwa na alama 46 nafasi ya nne sambambana na Azam FC.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.