Ads

ALIYEWAAMUA MAHASIMU WA JIJI LA MADRID APEWA ‘MANCHESTER DERBY’......

Muamuzi Mark Clatternburg amekabidhiwa jukumu la kupuliza filimbi katika mechi ya wapinzani wa jadi wa jiji la Manchester nchini England itakayochezwa siku ya Jumamosi.

Mwamuzi huyo alikuwa na majukumu makubwa sana msimu uliopita na aliyatendea haki ipasavyo, mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 41 alikuwa mwamuzi katika fainali ya klabu bingwa barani Ulaya msimu uliopita iliyozikutanisha timu mahasimu za jiji la Madrid nchini Hispania Real Madrid na Atletco Madrid, vilevile alikuwa na jukumu la kuamua mechi ya fainali kombe la FA baina ya Manchester United na Everton kabla ya kuchezesha fainali ya Euro baina ya Ureno na Ufaransa.

Wakati Clatternburg akiwa mwamuzi wa kati, Mike Dean yeye atakuwa na jukumu la kuwanyamazisha Pep Guardiola na hasimu wake Jose Mourinho mbapo ameteuliwa kuwa mwamuzi wa mezani na changamoto kubwa kwake ni kujipanga kukabiliana na mihemko kutoka kwa makocha hao wenye ushawishi mkubwa katika soka la dunia.

Hata hivyo Clatternburg itamlazimu kutumia uzoefu wake mkubwa kudhibiti nidhamu kwenye pambano hilo ambalo linagusa hisia za watu wengi i duniani.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.