Ads

Ohooo mmemsikia omong alichokisema!!!!!!



Image result for simba sport club photo

SIMBA imeianza Ligi Kuu Bara msimu huu kwa kishindo baada ya kuifumua Ruvu Shooting mabao 7-0 na kuiacha timu hiyo kileleni, lakini kama unadhani Simba wameridhika na ushindi huo pole, kwani Kocha Mkuu wake, Joseph Omog, amesema utamu zaidi unakuja.
Mcameroon huyo amesema ushindi huo ni ishara tosha kuwa mambo mazuri yanakuja katika timu yao, hivyo mashabiki wakae mkao wa kula na waache kulaumu wachezaji wao.
Omog alisema kwanza mechi hiyo imeingia katika historia yake ya soka tangu alipojiunga na kikosi cha Simba Julai 2016, kwani hakuwahi kupata ushindi mkubwa kama huo.
“Washambuliaji wangu wameanza kupokea vema maelekezo niliyokuwa nawapa tangu tukiwa kambini Afrika Kusini, naamini moto utawaka zaidi kadiri ligi itakavyosonga mbele,” alisema.
“Mashabiki na wapenzi wa Simba wanatakiwa watulie na kuacha kuwalaumu wachezaji, kwani siku zinavyozidi kwenda watafurahi kila mechi.”
BOCCO
AISUBIRI AZAM
Katika hatua nyingine, straika John Bocco ‘Adebayor’ amesajiliwa na Simba kutoka Azam na kuzikosa mechi za Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga na ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting.
Hata hivyo taarifa nzuri ni kwamba mchezaji huyo aliyekuwa akisumbuliwa na maumivu ya nyama za paja, sasa anaweza kuvaana na timu yake ya zamani wakati timu hizo zitakapopambana wiki ijayo.
Daktari wa Simba, Yassin Gembe, amesema Bocco anaendelea vizuri, lakini aliamua kumpumzisha katika mechi ya Ruvu Shooting ili kuweza kuimarika zaidi.
“Bocco anaendelea vizuri lakini kwa usalama zaidi nimemuongezea mazoezi binafsi ya peke yake ili kuweza kuwa fiti zaidi na mechi ambayo itakuwa ya kwanza kwake kimashindano akiwa na Simba itakuwa dhidi ya timu yake za zamani Azam,” alisema Dk Gembe.a

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.