Ads

Daaaah! kweli kiba kaliamsha dude....!!!!


Image result for alikiba


Kiongozi Mwingine ambaye aliwahi kuwa waziri wa Nishati na Madini Willium Ngeleja naye ameonekana kuguswa na wimbo huo na kuamua kumpongeza Kiba n kuandika Hivi kwenye Ukurasa wake wa Instagram

"King @OfficialAlikiba : Nyimbo ya Seduce me umeitendea haki tasnia ya muziki nchini pia utaitambulisha nchi yetu kimataifa. Hongera"

Mwingine ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi ameweka hisia zake hadharani kwa kumsifia Alikiba kwa uzuri wa wimbo wake  mpya wa ,Seduce me’ huku  akiahidi kumpatia zawadi yoyote aipendayo

Mhe. Hapi ameshindwa kuzuia hisia zake juu ya wimbo huo mpya wa Alikiba ikiwa ni siku chache zimepita tangu msanii huyo aachie ngoma hiyo  baada ya kukaa mwaka 1 na miezi kadhaa tangu alipotoa wimbo wake wa Aje .

“Nimekuelewa sanaa wajina @officialalikiba. Kazi imeenda shule.Nidai zawadi kwa muziki huu wa ukweli.Keep the fire burning!”,ameandika Mhe Ally Hapi.

Wimbo huo ambao tayari umeshavunja rekodi ya kutazamwa zaidi kwenye mtandao wa Youtube nchini Tanzania unaonekana kuwavutia mastaa kibao hapa nchini akiwemo Wema Sepetu.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.