Ads

WAANNE WAPATA ZALI SIMBA



Image result for simba sport club photo

Image result for advertise here

WAKATI straika, Juma Liuzio ‘Ndanda’ akiwachunia viongozi wa Simba kwa kugoma kwenda kambini Afrika Kusini, mastaa wanne wa timu hiyo wamejikuta wakipata zali bila kutarajia.
Wachezaji hao wale wapya waliosajiliwa katika kikosi hicho msimu huu ambao bila kutarajiwa wamejikuta wakipandishwa ndege na kusafirishwa kwenda Bondeni kwa ajili ya kambi ya timu hiyo.
Nyota hao walisafiri na kikosi cha Simba alfajiri ya jana Jumatatu kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa mashindano wakitarajiwa kutambulishwa rasmi siku ya Simba Day.
Wachezaji hao walioangukiwa na zali hilo ni kipa Emmanuel Mseja na beki wa kushoto Jamal Mwambeleko waliotoka Mbao FC iliyopanda Ligi Kuu Bara msimu uliopita na kunusurika kushuka daraja.
Wengine waliopata zali hilo bila kutegemea ni beki wa kati, Yusuph Mlipili aliyetokea Toto Africans na kiraka Ally Shomary aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar walikwea pipa kwa mara kwanza jana kwenda nje ya nchi.
Nyota hao wamesajiliwa katika usajili wa sasa chini ya kocha Joseph Omog ambaye amepania kuipa Simba ubingwa katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Simba imeweka kambi nje ya nchi kwa mara ya kwanza tangu Oktoba 2014 ambapo ilichimbia pia nchini humo wakati ikijiandaa na mchezo dhidi ya watani zao Yanga ambao ulimalizika kwa suluhu.
LIUZIO AAMUA
KUUCHUNA
Wakati nyota hao wanne wakiendelea kujishangaa kwa zali lililowapata, straika Juma Liuzio ‘Ndanda’, amewawekea ngumu viongozi wa Simba kwa kugoma kuungana na timu hiyo Afrika Kusini.
Liuzio aliyeichezea Simba kuanzia dirisha dogo la usajili wa msimu uliopita kwa mkopo akitokea Zesco Fc ya Zambia, alisema ameshindwa kuondoka na wenzake kwa vile hajasaini mkataba mpya wa kuwa mchezaji rasmi wa Simba.
Straika huyo alisema licha ya mabosi wa Simba kumkatia tiketi, aliamua kugoma kuondoka kwa sababu yeye si mchezaji halali wa timu hiyo.
Nyota huyo aliyewahi kucheza Mtibwa Sugar, alisema hawezi kujifua na timu hiyo wakati hawajakubaliana katika mazungumzo ya mkataba mpya.
“Sikwenda Afrika Kusini, na hata viongozi walipoona sijafika uwanja wa ndege, walinipigia simu kujua nipo wapi, nikawajibu sitaenda kwani si mchezaji halali kwa kuwa mkataba wangu wa mkopo ulimalizika,” alisema Liuzio.
“Kuna kiongozi kanipigia simu kwamba niende tukaongee, hii ni baada ya kukataa waliponiambia nitasaini nikitoka Afrika Kusini,” alisema Liuzio aliyeibuliwa na Polisi Morogoro kabla ya kudakwa na Mtibwa.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.