TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMANNE 18 JULY 2017 na Ally mshana
Mabingwa wa England, Chelsea wana "nia thabiti" ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, 29. (Sky Sport)
Chelsea wanazungumza na Manchester City kuhusiana na usajili wa Sergio Aguero. (beIN Sporst)
Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovic hayuko tayari kulipa fedha nyingi kumsajili Alvaro Morata, 24, kutoka Real Madrid, huku kukiwa na taarifa kuwa mchezaji huyo anaelekea Italia. (Star)
Chelsea wanafikiria kumrejesha tena Stamford Bridge, beki wa Southampton Ryan Bertrand. (Evening Standard)
Chelsea wanataka kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang. (Sky Sports)
Dau la pauni milioni 2.6 la Manchester City kumtaka kipa wa Napoli, Pepe Reina, 34, limekataliwa. (Mirror)
Manchester City hawatakabiliwa na ushindani tena kutoka Bayern Munich katika kumsajili Alexis Sanchez, 28, kutoka Arsenal baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge kusema hawamfuatilii tena. (Manchester Evening News)
Paris Saint-Germain wameingia katika mbio za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Alexis sanchez, 28. (Daily Mirror)
Paris Saint-Germain wapo tayari "kuvunja benki" kutaka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Neymar, na watakuwa tayari hata kulipa euro milioni 222, kulazimisha uhamisho wake. (GianlucaDiMarzio.com)
Washauri wa karibu wa Neymar wanamshauri aondoke Barcelona ili kuepuka kufunikwa na Lionel Messi. Manchester City, PSG na Manchester United zote zinamtaka mshambuliaji huyo kutoka Brazil. (Sport)
Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona amesema hakuna timu itakuwa tayari kutoa pauni milioni 195 kumsajili Neymar, 25. (Mail)
Manchester United wanafikiria kupanda dau la mwisho la pauni milioni 60 kumtaka kiungo wa Tottenham, Eric Dier, 23. (Mirror)
Zlatan Ibrahimovic, 35, ameonesha dalili kuwa atabakia Old Trafford baada na kuwaandikisha watoto wake katika akademi ya Manchester United. (Sun)
Manchester United wanamtaka kiungo anayesakwa na Liverpool Naby Keita, 22, huku klabu yake RB Leipzig ikipunguza vikwazo. Mbali na United na Liverpool, pia Arsenal, Manchester City, Juventus na Inter Milan zinamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Guinea. (Football Whispers)
Manchester United wana uhakika wa kukamilisha usajili wa Ivan Perisic katika saa 48 zijazo. (Starsport)
West Brom wanamtaka beki wa Arsenal Kieran Gibbs, 27, lakini timu hizo mbili hazijafikia makubaliano yoyote. (Birmingham Mail)
Arsenal watajaribu kupunguza idadi kubwa ya wachezaji wake wasiotumika, kabla ya kufanya uamuzi wa kuvunja rekodi tena ya usajili na kumchukua Thomas Lemar, 21, kutoka Monaco. (Mail)
Monaco wamewaambia Arsenal watalazimika kuvunja rekodi yao ya usajili kwa kutoa takriban pauni milioni 80 kumsajili kiungo Thomas Lemar, 21. (The Mirror)
Arsenal wamekataa dau la pauni milioni 6.2 kutoka Sampdoria la kutaka kumsajili kiungo Jack Wilshere, 25. Arsenal wanataka pauni milioni 8.8. (DI Marzio)
Juventus wanataka kuimarisha kiungo chao kwa kumsajili Nemanja Matic, 28, au Steven N'Zonzi, au William Carvalho. (Calciomercato)
Inter Milan wanapanga kuwajaribu Real Madrid kwa kutoa dau kubwa kumtaka kiungo Toni Kroos. (Sport Mediaset)
Crystal Palace wanakaribia kumsajili beki wa Ajax, Jairo Riedewald, 20 kwa pauni milioni 8. (Evening Standard)
Crystal Palace wanataka kuimarisha kiungo chao kwa kumchukua Jack Wilshere kutoka Arsenal kwa mkopo. (The Sun)
Crystal Palace wapo tayari kutoa pauni milioni 16 kumsajili beki wa Arsenal Callum Chambers, 22. (Telegraph)
Beki wa kushoto wa Nice ya Ufaransa Dalbert Henrique, 23, amethibitisha kuwa Liverpool wanamtaka, lakini amesema dau kutoka Inter Milan ni la kuvutia zaidi. (Express)
Riyad Mahrez, 26, yuko tayari kupunguziwa mshahara ili aweze kujiunga na Roma. (Leicester Mercury)
Kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny, 27, anakaribia kujiunga na Juventus. (Guardian)
Winga wa Hull City, Ahmed Elmohamady, 29, anakaribia kujiunga na Aston Villa. (Hull Daily Mail)
Beki wa kushoto wa Hull City Andy Robertson, 23, anakaribia kujiunga na Liverpool kwa pauni milioni 8. (Liverpool Echo)
Mshambuliaji wa Manchester City Wilfried Bony, 28, hajasafiri na kikosi kilichokwenda Marekani na huenda akarejea tena Swansea. (Wales Online)
Beki Matheiu Debuchy wa Arsenal anatarajiwa kujiunga na Nice ndani ya saa 48 zijazo, baada ya kushindwa kuwika Emirates. (Europe1 Sports)
No comments