Ads

SINGIDA HATUMTAKI BOSUNGU...



Image result for busungu yanga

 Beki wa kati wa Yanga, Vicent Bossou baada ya kumalizika kwa mkataba wake alikuwa akihusishwa na taarifa za kujiunga na Singida United ambayo inanolewa na Mdachi Hans Van Pluijm  aliyekuwa kocha wa Yanga.
Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga alisema kuwa mwanzoni walikuwa na mipango na mchezaji huyo, lakini baada ya kufanya usajili wa wachezaji wa kigeni katika kikosi hiko waliamua kuchana naye.
Sanga alisema kuwa baada ya kufanya usajili walijikuta wanatimiza julma ya wachezaji saba wa kigeni kama kanuni ya ligi inavyosema na kuamua kuachana rasmi na jina la mchezaji huyo ingawa alikuwa ni moja ya mchezaji waliyokuwa wakimuhitaji..
"Tushakamilisha jumla ya wachezaji saba wa kigeni katika kikosi chetu, kwahiyo hatutakuwa tena na mahitaji na Bossou ingawa alikuwa yupo katika mipango yetu," alisema Sanga.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.