Ads

DANTE,KWASIMBA HII MBONA KAZI IPO...



Image result for dante yanga

BEKI wa Yanga, Andrew Vicent ‘Dante’, amekichunguza kikosi cha Taifa Stars inayoshiriki michuano ya Cosafa nchini Afrika Kusini na kubaini nyota wa Simba ndiyo wameishika timu hiyo jambo ambalo linaweza kuwagharimu Yanga kwenye mchezo wa Ngao ya Hisani mwezi ujao.
Simba na Yanga zitakutana katika mechi ya Ngao ya Jamii Agosti 19, kwenye Uwanja wa Taifa, kitu ambacho kimempa hofu Dante ambaye amegundua kuwa nyota muhimu wa Simba wako moto kwenye kikosi cha Stars.
Nyota wa Simba ambao wako Sauzi na kikosi cha kocha Salum Mayanga ni Aishi Manula, Shomary Kapombe, Shiza Kichuya na Mzamiru Yasin huku John akiongezwa kwaajili ya michua CHAN.
“Tayari wamepata uzoefu katika timu zinazoshiriki michuano ya Cosafa, wakija watakuwa na vitu vipya, wakati Yanga, wanaoonekana kutumika ni Simon Msuva na Raphael Daud ambaye amecheza baadhi ya mechi,”alisema.
Dante alikwenda mbali na kusema kuwa mechi hiyo ya Ngao ya Jamii itakuwa ya aina yake, kutokana na Ibrahim Ajibu kutua Yanga na Simba kumrejesha Emmanuel Okwi ambaye kuifunga Yanga haijawahi kuwa tatizo kwake.
“Hakuna kitu kigumu kama mashabiki kusubiri jambo fulani kutoka kwa mchezaji anayezungumzwa sana mtaani. Mfano kila kona walipo Mashabiki wa Simba wimbo ni Okwi na Manula, huku Yanga ni Ajibu, hilo litakusanya nyomi ya watu taifa, kuwashuhudia,” alisema
Staa wa zamani wa Yanga, Sekilojo Chambua, naye alitoa mtazamo wake kuhusiana na mechi hiyo kwamba itakuwa na vitu viwili muhimu vitakavyokuwa kivutio kwa mashabiki.
“Cha kwanza ni usajili, kwa maana ya kuwaona nyota wao kabla ya ligi kuanza, kisasi cha Ajibu dhidi ya Simba na Okwi kurejea kwenye klabu yake hiyo ya zamani itakuwa ni kivutio cha aina yake mbele ya watazamaji,” alisema Chambua.     

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.