Ads

KWELI SIMBA YA MSIMU HUU IMEAMUA




Image result for advertise here




Image result for nicholas gyan

ENDAPO Simba itafanikiwa kunasa saini ya straika mpya raia wa Ghana, Nicholas Gyan itakuwa imelamba dume kutokana na ubora wa mchezaji huyo imefahamika.


Taarifa kutoka jijini Accra inaeleza kuwa Gyan ambaye ni mdogo wa Asamoah Gyan, nyota na nahodha wa timu ya Taifa ya Ghana ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu ya nchi hiyo msimu uliomalizika hivi karibuni.

"Pia ndiye mfungaji bora wa msimu uliomalizika, kwa sasa ana umri wa miaka 19 na ikifika Desemba 23 mwaka huu atafikisha miaka 20, kwa wachezaji huu ndio umri wa kuonyesha makali yake," kilisema chanzo chetu.

Taarifa zaidi kutoka klabu ya Simba zilisema kuwa straika huyo alitarajiwa kutua nchini kati ya jana usiku na leo akiwa sambamba na Kaimu Makamu wa Rais , Iddi Kajuna, ambaye alikwenda Ghana kukamilisha usajili wa straika huyo kinda.

Akizungumza na gazeti la Nipashe jana, mmoja wa viongozi wa Simba ambaye jina tunalihifadhi alisema kuwa klabu imedhamiria kusajili kikosi imara ambacho kitafanya vizuri kwenye ligi ya ndani na mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho watakayoshiriki mwakani.

"Tunataka kuamsha furaha na kuleta makombe mengi klabuni, tumezingatia mapungufu ya msimu uliopita, Simba tunayoifikiria ni ile inayoendana na ukubwa na hadhi ya klabu, tunataka kusonga mbele ," alisema kiongozi huyo wa juu.

Aliongeza kuwa katika utawala wake hataki kuona "maneno mengi" ila anataka vitendo viongee.

Alisema pia klabu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali watahakikisha tamasha la Simba Day mwaka huu linakuwa la kimataifa sambamba na shughuli nyingine za kijamii zitakazofanyika kuanzia Agosti Mosi.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.