Ads

KAULI YA JPM YAMUIBUA MH, MWANTUM MAHIZA...



Image result for mwantumu mahiza

Kauli ya Rais John Magufuli kuhusu wanafunzi wanaopata mimba kutoendelea na masomo katika shule za umma, imemuibua Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika Serikali ya Awamu ya Nne, Mwantumu Mahiza ambaye amempa pole kiongozi huyo wa nchi.


Mahiza ambaye ni Skauti Mkuu, alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya miaka 100 ya Chama cha Skauti Tanzania yatakayofanyika mjini Dodoma Julai 26.

 “Nampa pole Rais, mwaka 2010 tulikaa vikao na viongozi wa wizara ya elimu na wa taasisi za dini, tulishindwa kufikia muafaka juu ya wanafunzi waliopata mimba kuendelea kusoma, hivyo anatakiwa kulitazama  kwa undani,” amesema Mahiza.

Amesema wakati wakijadili suala hilo, Wizara ya Afya ilikuwa ikipambana na vifo vitokanavyo na mimba za umri mdogo hospitalini.

Mahiza alisema wakati huohuo, viongozi wa dini walisema suala la mwanafunzi kupata mimba na kurudi shule litavunja maadili ya dini.

“Kwenye vikao wengine walikuwa wanajadili wanafunzi hao wataitwa akina nani shuleni maana wameshazaa,” amesema.

Waziri huyo wa zamani amesema asilimia 0.09 walikuwa ni wanafunzi ambao hawataki kwenda shule bila sababu na  asilimia 0.06 walikuwa ni kutoka familia duni.

Mahiza amesema asilimia 90 walikuwa ni wanafunzi ambao hawakuwa na mahitaji muhimu ya shule ikiwamo sare na madaftari.

Amesema jambo hilo ndilo lililosababisha Serikali mwaka 2006/2007 kuanzisha shule za kata ili kupanua wigo kwa wanafunzi kupata elimu.

Mahiza amesema ili kukabiliana na mimba kwa wanafunzi, wazazi wapambane kupunguza mmomonyoko wa maadili kakita familia.

“Nawaomba wazazi tushirikiane kuhakikisha watoto wanakuwa na maadili mazuri kuanzia shuleni mpaka nyumbani ili wapate elimu,” amesema Mahiza.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.