Ads

KASEKE NA YANGA BANDO HAKIJAELEWEKA


Image result for kaseke yanga

KIUNGO Deus Kaseke huenda asiichezee klabu yake ya Yanga msimu ujao baada ya kushindwa kuafikiana katika makubaliano yao.


Kaseke alirejea Dar es Salaam Alhamisi kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kusaini mkataba mpya baada ya uongozi wa klabu hiyo kushtukia dili la Singida United kutaka kumsainisha kiungo huyo ambaye mkataba wake Yanga unamalizika mwishoni mwa mwezi huu.

Mmoja wa viongozi wa klabu ya Yanga, ambaye hakutaka jina lake liandikwe , aliliambia gazeti la Nipashe kuwa pande hizo mbili bado hazijaafikiana kimazungumzo baada ya Kaseke kutaka kulipwa milioni 45 ili asaini mkataba wa miaka miwili kiasi ambacho Yanga bado wamekuwa wazito kukubaliana.

“Uongozi wa Yanga upo tayari kumpa Kaseke milioni 25, lakini mchezaji amesisitiza hayupo tayari kusaini mkataba kwa pesa hizo, kwa hiyo bado hakuna uhakika kama atasaini mkataba mpya na Yanga ama la,” alisema kiongozi huyo.

Aidha, alisema kama watashindwa kuafikiana, ni wazi nyota huyo hatokuwa sehemu ya kikosi cha Yanga msimu ujao.

Nyota huyo amekuwa akiwindwa na klabu ya Singida United kufuatia kocha wa timu hiyo, Mholanzi Hans van Pluijm kuushauri uongozi wa timu hiyo kumsajili.

Katika hatua nyingine, kikosi cha timu hiyo hakikuanza mazoezi jana kama ilivyoelezwa na badala yake kinatarajia kuanza leo.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.