GIGY MONEY AKIRI KUTOA MIMBA MBILI...
MUUZA sura kwenye video za wasanii Bongo, ambaye mwili wake ‘umepukutika’ ghafla, Gift Stanford maarufu kama Gigy Money, amekiri kutoa mimba mbili mfululizo ambazo ndizo zilizosababisha hali hiyo.
Akizoza na Za Motomoto News, muuza nyago huyo ambaye awali alionekana kuwa na kalio lililotesa mioyo ya wakware wengi, alisema kitendo cha kutoa mimba hizo kilimfanya kuwa taaban na chupuchupu akumbwe na mauti.
“Roho inaniuma sipendi kuongea haya, lakini ni kweli nilinasa ujauzito mara mbili mfululizo, kutokana na vipigo vya mwanaume niliyekuwa naye,… (anamtaja jina) mimba zikawa zinatoka, ya mwisho hadi kizazi kilitoka nje nikaumwa sana hadi nilijua nakufa nikalazwa hospitali siku mbili,” alisema msanii huyo.
No comments