AJIBU RASMI JANGWANI....
Dar es Salaam. Baada ya kuwepo kwa tetesi za muda mrefu, straika Ibrahim Ajib amesaini rasmi mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga ambayo ndiyo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu.
Ajibu amesaini mkataba huo leo mbele ya mabosi wa Yanga na kutambulishwa rasmi kwa mashabiki wa klabu hiyo.
Nyota huyo anakuwa mchezaji wa pili kusainiwa na Yanga katika usajili wa sasa huku klabu hiyo ikiwa mbioni kukamilisha usajili wa kiungo wa Mbeya City, Raphael Daudi.
No comments