Ads

ASIKUAMBIE MTU KUMBE MRITHI WA AJIBU YUPO BWANA....



Image result for mohamed ibrahim simba


PAMOJA na Simba kufanya usajili wa nyota kadhaa ikiwemo aliyekuwa nahodha wa Azam, John Bocco, nyota wa zamani wa timu hiyo wamemtaja mshambuliaji Mohammed Ibrahim kuwa ndiye mrithi sahihi wa Ibrahim Ajibu aliyehamia Yanga.
Winga wa zamani wa Simba, Ulimboka Mwakingwe alisema: “Ibrahim anaweza kuwa mchezaji sahihi ambaye anaweza kucheza nafasi hiyo kwa uwezo na ufanisi mkubwa tena zaidi ya alivyokuwa anafanya Ajibu, na akaisaidia Simba kupata matokeo ya ushindi.”
Beki kisiki wa zamani wa Simba, Boniface Pawasa yeye alisema: “Simba wana wachezaji kama Mohammed Ibrahim na Said Ndemla, kama wakipata nafasi na kuaminiwa kwa kiasi kikubwa, wana uwezo mkubwa wa kucheza nafasi ya kiungo na wakafanya kazi vizuri ambayo ni zaidi iliyokuwa ikifanywa hapo awali.”
Pawasa alisema kuwa alitamani kumwona Ajibu anakwenda kucheza soka nje ya nchi kama alivyokuwa akitakiwa katika nchi za Misri na Afrika Kusini na si kubaki hapa nchi kama alivyoamua kusaini Yanga.
LUFUNGA BADO
Beki msomi wa Simba, Novatus Lufunga yuko njia panda hajui ni wapi atakuwepo msimu ujao licha ya kuwa mkataba wake na Simba utamalizika mwezi Desemba.
Lufunga aliyesajiliwa na Simba akitokea Mgambo ya Tanga, amekwenda Mwanza kwa mapumziko na kufanya mambo mengine, lakini hajajua ni wapi atakuwa.
Akizungumza na Mwanaspoti, Lufunga ambaye anacheza beki ya kati na alikuwa pamoja na Mzimbabwe Method Mwanjali na Mganda Juuko Murshid, alisema: “Niko kwenye mapumziko kwa sasa, yaani mambo ya msimu ujao hata sijui itakuwa vipi yaani niko napumzika.
“Ni mchezaji wa Simba, lakini tunaanza msimu mpya sijui kama nitaendelea na hapo au nitakuwa mahali pengine yote ni mipango, mambo hayo ni ya baadaye kwa sasa napumzika.”

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.