Kweli mwenye nguvu mpishe apite Simba,Azam na yanga....
Review...
Klabu za Simba,Yanga na Azam zimeendelea kuibomoa Mbao FC kwa kuendelea kuchukua wachezaji wa timu hiyo iliyopanda daraja msimu uliopita.
Pigo jipya kwa Mbao FC limetokea mwishoni mwa wiki baada ya Azam kumsajili kipa wake Benedict Haule kwa kusaini mkataba wa miaka mwili.
Mbao iliyofanikiwa kucheza fainali ya Kombe la FA, tangu wakati huo nyota wake wameanza kuangaliwa kwa jicho la karibu na Simba,Yanga na Azam, huku wengine wakiendelea kunyatiwa kimyakimya na klabu nyingine.
Wachezaji waliondoka hadi sasa ni kiungo mshambuliaji, Pius Buswita (Yanga), Jamali Mwambeleko (Simba), Salimin Hoza na Benedict Haule (Azam).
Wachezaji wengine wanaotarajiwa kuondoka klabu hapo ni pamoja na beki Yusuph Ndikumana anayewaniwa na Simba na Yanga.
Kipa Haule alisema sasa anaanza maisha mapya ili kupata changamoto mpya Azam.
Alisema kuwa yeye kazi yake ni soka, hivyo kujiunga na Azam na kuziacha Mbao na Majimaji ambazo zilikuwa zinamuhitaji hajafanya makosa kwani zilishindwa zenyewe.
“Nimejiunga na Azam kwa mkataba wa miaka miwili, ni changamoto kwangu kusaka maisha sehemu nyingine, niseme kwamba hata huku (Azam) sijakosea,” alisema kipa huyo.
Mwenyekiti wa Mbao FC, Sory Njashi alisema wanawatakia maisha mema wale wote ambao wameihama timu yao na kwamba wataandaa kikosi kingine kipya.
“Sisi tunawatakia kila la kheri, Mbao itaendelea kuwapo na tutajipanga tena kuwaandaa vijana wengine katika msimu ujao..hatuna wasiwasi,” alisema Njashi.
No comments