Ads

Guardiola amenza na Kyle Walker....


Image result for kyle walker

Klabu ya Manachester City imeanza mazungumzo na mchezaji wa Tottenham Hotspur, Kyle Walker.
Kocha Pep Guardiola ambaye kikosi chake kilimaliza nafasi ya tatu msimu ulioisha, anajipanga kuhakikisha anaimarisha kikosi chake.
Dirisha hili la usajili ndiyo njia ya Guardiola kuendeleza kampeni yake ya kuiamarisha kikosi chake msimu ujao.
Imeelezwa kwamba uhamisho wa mchezaji huyo utafanyika baada ya England kucheza na Ufaransa kwenye mechi ya kirafiki ya kimataifa, huku Guardiola akijihakikishia kwamba lazima amsajili mchezaji huyo.
Mchezaji Walker alisajiliwa Spurs Septemba mwaka jana kwa mkataba wa miaka mitano hadi mwaka 2021, hivyo kibarua kigumu kitakuwa kwa Guradiola kwenda kumshawishi Maurcio Pochettino.
 Guardiola ameongeza juhudi za kumsaka mchezaji huyo baada ya kumwachia Pablo Zabaleta kwa West Ham
Mchezaji huyo ametengewa dau la Pauni 40 milioni licha ya Spurs kutangaza Pauni 50 milioni iwapo wanataka kumtoa klabuni hapo.
Ushawishi wa Guardipla ukigonga mwamba kwa mchezaji huyo, atalazimika kuvunja benki ili kufukia dau waliloweka.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.