Ads

TETESI NA HABARI ZA USAJILI KUTOKA LIGI KUU UINGEREZA, LA LIGA, SERIE A, BUNDESLIGA NA KWINGINEKO WIKI HII


Pepe Real Madrid Atletico Madrid La Liga
Beki mahiri wa Real Madrid Pepe amekataa kujiunga na klabu za China kwa sababu anataka kwenda Inter Milan, kwa mujibu wa Marca.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno anatarajia kuondoka La Liga mwisho wa msimu huu PSG na Hebei Fortune zikiwa zinaitamani saini yake.

BAYERN YAWAFUKUZIA ALEXIS & VERRATTI

Marco Verratti PSG Montpellier
Bayern Munich wapo tayari kutoa kitita cha euro milioni 120 kuwanasa Marco Verratti na Alexis Sanchez majira ya joto kwa mujibu wa jarida la Bild.
Kiungo huyo wa Kiitaliano amekuwa akifuatiliwa na Barcelona, lakini uhusiano wake wa karibu na bosi wa Bayern Munich, Carlo Ancelotti unaweza kuwapatia miamba hao wa Bavaria fursa ya kumsajili mbele ya Barca kwa euro milioni 60.
Kwa upande mwingine Bayern bado wanaitamani saini ya Alexis Sanchez na watalipa euro milioni 60 nyingine kwa ajili ya nyota huyo wa Arsenal.

MAN UTD WANALO DAU KUMSAJILI JAMES

James Rodriguez Real Madrid La Liga
Manchester United tayari wameshatoa dau nono kwa ajili ya kiungo wa Real Madrid James Rodriguez majira ya joto, kwa mujibu wa RCN Radio.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia amezidi kukasirishwa na kukosa namba kikosi cha kwanza Real Madrid chini ya Zinedine Zidane.

LIVERPOOL KUMSAJILI RONALDINHO MPYA

Luan Guilherme de Jesus Vieira Gremio
Jurgen Klopp anakaribia kukamilisha dili jipya kumsajili nyota wa Kibrazili Luan kwa kitita cha paundi milioni 26, ambaye amebatizwa jina la 'Ronaldinho Mpya', kwa mujibu wa Mirror.
Liverpool wamekuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu mchezaji huyo wa Gremio mwenye umri wa miaka 24 na wawakilishi wake wamefanya mazungumzo na Reds mwezi uliopita.

ATLETICO MADRID YAPANGA KUMSAJILI VARDY

Jamie Vardy Leicester City Champions League
Atletico Madrid wamejipanga kumsajili mshambulizi wa Leicester City Jamie Vardy, Sky Sports limeripoti.
Diego Simeone ataendelea kubaki Vicente Calderon na miamba hao wa Hispania bado wangali wakipambana na rufaa dhidi ya adhabu yao ya kufungiwa usajili ili waweze kumnasa nyota huyo.

CHELSEA YAMFUKUZIA NYOTA WA KIJERUMANI

Jann-Fiete Arp Germany
Chelsea ni miongoni mwa klabu za Ulaya zinazomfukuzia kinga wa Hamburg, Jann-Fiete Arp, Kwa mujibu wa Bild.
Nahodha huyo wa timu ya Ujerumani chini ya miaka 17 amevutia wengi kwa kiwango chake kimataifa, akiwa amefunga hat-trik mbili kwa nchi yake kwenye michuano UEFA-17 huko Croatia.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.