Ads

BONGO MOVIE MNALOGANA WENYEWE KWA WENYEWE.......................

                                    

    MAKALA
                          
                              
                        BONGO MOVIE
Image result for bongo movie

Miezi michache waziri wa utamaduni, sanaa na michezo aliamua kutangaza kuwa ni marufuku kwa wauzaji wa filamu hapa nchini kuuza filamu za kigeni(kuzifungia) na kusema atakayekamatwa atawajibika.

         Lakini Mh waziri huwa naamini siku zote kiongozi wa familia akiwa na maadili mazuri basi hata familia yote inampenda na kumfuata.huwezi ukakataza filamu za wenzetu kuuzwa ndani ya nchi yako ila ungejiuliza ni kwa nini filamu za nje zinauzika sana ndani ya nchi yako na kwa nini filamu za nchi yako hazina soko ndani ya nchi yako halikadhalika nje ya nchi.


  • Mh  sikukosoi kwa maamuzi yako ila wakati mwingine ushauri nao unanafaida yake.
Hivi nikweli unaweza kulalamika unaonewa alafu hakuna mtu wa kukusikiliza na akajitokeza mtu wa kukusikiliza ila akaona unacholalamika ni ujinga? basi ukweli nikwamba BONGO MOVIE kabla hamjaanza kulalamika kuwa kazi zenu haziuziki basi mngepaswa kujiuliza maswali mengi na kusingekuwa na haja ya kulalamika.

  • Tatizo kubwa liko kwenye maudhui ya movie zenu kwani unadhani hamjui mnajua sana ila bado hamjaamua kushughulisha vichwa vyenu nakufanya kitu kama wenzenu wa huko KOREA,CHINA,JAPAN,na INDIA.

Ukweli uko hivi sikuzote hakuna mtu anayefundishwa mapenzi na filamu zenu nyingi zinahusisha mapenzi sana wakati zipo aidia nyingi ambazo mkikaa na kuzifanyia kazi mnazalisha kitu ambacho kitawafanya kuuza kazi zenu.Et "Sababu kubwa inayofanya filamu zetu(movies) zisiuzike ni MKOREA, MUHINDI, MCHINA, JAPAN kweli ndo chanzo lakini jiulizeni kwanini sasa iwe hvyo.

  1. Kwa upande wa India lazima Filamu zake(movies) zake ziuzike kwa wingi kutokana na ubora wa filamu zenyewe na hii inatokana na maandalizi ya muda mrefu wa filamu hizo.Pale indi kuna vikundi vyingi vya sanaa vikiwa na wasanii maarufu na wengine wanao chipukia wote waliamua kukaa na kuunda chama chao cha filamu kinachojulikana kama "BOLLYWOOD".
Image result for udan indian drama

Ukweli uliopo wazi ndani ya chama hiki nikwamba wasanii wanapangiwa majukumu na kila "DIRECTOR"anapewa idadi ya wasanii ili kutengeneza filamu(movie) ambapo filamu inaweza kuchukua miaka zaidi ya miwili kukamilika.Nahii lazima mtazamaji ajifunze kitu, mfano mzuri ni ile filamu ya 'KAL HO NA HOO" ya  muigizaji maarufu wa India SHUR KHAN.Pia movie nyingine kama UDAN

Achana na India kuna hawa jamaa ambao hata Marekani kwa umaarufu wake wa Filamu  bado anamsumbua kichwa, KOREA ni moja ya nchi ambayo ilikuwa nyuma sana kwa upande wa uigizaji wa filamu, lakini hawa ndio chanzo cha malalamiko ya wasanii wa Bongo Movies kuaza kulalamika kuwa kazi zao haziuziki.

Unawaeza kujiuliza kwanini hata Marekani anamkubali Mkorea ila ukweli upo wazi mana sio Marekani pekeyake hata mimi ukiniuliza ni filamu(movie) gani ninayoipenda lazima nitaanza na ile ya "GIANT" ndo nije hapa kwetu "BADO NATAFUTA" na hii yote inatokana na ubunifu na ubora wa filamu zao.


          2. Kwa pale korea kuna kampuni mbili ambazo ni maarufu na zimekuwa zikisapoti filamu za chini hapo.Kuna "GOOD DRAMA NET" na DRAMA GO.COM.Hizi ni kampuni ambazo zimetoa Filamu(movies) kama vile, East of eden, Moorim School, Giant, Blood na nyingine nyingi ambazo zimekuwa zikiuzika ndani na nje ya nchi ya Korea.

Image result for giant korean drama

Sasa jiulizeni wenzenu wanatoa movie na zinakubalika kwao na hata kwenu nyinyi mnakosea wapi?
  • Kwa hapa Tanzania kuna kampuni za filamu kubwa ikiwa ni "STEPS INTERTAIMENT" licha ya hapo vipo vikundi vya uigizaji kama vile "MZIMUNI THIETA" na vinginevyo.Lakini tatizo ni kwamba uwezeshaji ni mdogo pia kila msanii anataka atoke(kufanikiwa) peke yake kitu ambacho kinapelekea sanaa na tasnia kwa ujumla kuyumba.
Yupo mtu wa kukumbukwa na kuigwa katika tasnia hii ya filamu marehemu "STEVEN KANUMBA" kwani hadi hapa tulipofikia mchango wake ni mkubwa na mpaka sasa hakuna aliyefanya mambo kama aliyowahi kuyafanya kipindi cha uhai wake,kwani alikuwa ni mtu ambaye hana ubaguzi kwa wasanii wakubwa hata wale wadogo.Kwa mfano Filamu ya "JENIFA", "UNCLE JJ", "DAR TO LOGOS", "HERO OF THE CHURCH", "SUTURDAY MORNING" na nyngine nyingi.Kwenye baadhi ya Filamu zake alijitahidi kuwaweka wasanii wadogo ambao leo hii ni maarufu kama vile Elizabeth Lulu, Jenifa...Kweli mungu amlaze mahala pema.

Image result for bado natafuta
  • Waswahili wanasema hivi hata mchele uwe na mchanga kiasi gani huwezi kuumwaga utauchambua mana ni wakwako ili usife na njaa.lazima mkubali kuwa hawa jamaa sana sana MKOREA,JAPAN na MCHINA wanaweza zaidi yenu kaeni mjifunze kutoka kwenye filamu zao.Kivipi sasa mtafanya vizuri? jibu liko wazi sio lazima msanii(mwigizaji) atake atake kufanikiwa peke yake cha msingi ni kuungana na kufanya good production.
Mfano mzuri ni huu hapa "mnakumbuka kipindi kile cha filamu ya 'JUMBA LA DHAHABU' pale alikuwepo mzee Chilo,Jini kabula, Chuz(Chuzday Kihangala),Basupa,Mzee khan kaa,SnuraJoan,Bella na mastaa wengi.Filamu hii ilipendwa na kila mtu alipenda kutokana na maudhui yaliyokuwepo pale ndani ikiwemo usaliti,chuki,wivu,mapenzi,visasi........
  • Turudi tena kwa wamarekani kuna filamu(movie) ambayo imeuzwa Marekani pia nchi nyingine kutokana na ubora wake"FAST AND FARIOUS"pale yupo marehemu paul walker,The Rock,Van dezo,Joson Statham na mastaa wakubwa tu wa marekani ambao waliamua kutoa umaarufu wao na wakafanya good production.

Image result for jumba la dhahabu

UKWELI NI HUU BADO MSIMTAFUTE MCHAWI WAKATI MNAJILOGA WENYEWE.HUWEZI KULALAMIKA KUWA UNAONEWA WAKATI UGOMVI ULIUANZISHA MWENYEWE.BONGO MOVIES BADO MKO CHINI BADO HAMJACHELEWA MNAWEZA KUKAA NA KUZIANGALIA MOVIE ZA JAMES BONDY ALAFU MKAONA MNAKOSEA WAPI.
Image result for james bond




Naomba kwa leo niishie hapo ila ikumbukwe kuwa kaulimbiu ya awamu ya tano inasema hapa kazi tu, inamaana kuwa kila mtu anatakiwa awe na kazi na hii nikuepusha vitendo vya kiuhalifu  ndani ya nchi. Na ukiangalia asilimia 85% ya vijana walishaanza kujiajiri kwa kuuza filamu hizo kwenye baadhi ya maeneo wengine wakitembeza mitaani.lakini waziri ameamua kuchukua maamuzi ya kuzifungia.

              Sasa swali nikwamba nini maana ya hapa kazi tu?
             Et Mh vitendo vya kihalifu vikizidi mitaani ndio vizuri?
              

IMEANDALIWA NA ALLY MSHANA.......24HOURSFORUM.BLOGSPOT.COM



No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.