Ads

Sidiria inayoweza kugundua saratani ya matiti............

Sidiria inayoweza kugundua dalili za saratani ya ugonjwa wa matiti


Haki miliki ya picha

Kijana mmoja nchini Mexico amevumbua sidiria inayoweza kugundua saratani ya matiti.
Lakini je sidiria hiyo inafanya kazi? Na iwapo inafanya ,inafanya vipi?.
Juliana Rios Cantu mwenye umri wa miaka 18 ametengeza sidiria ambayo anasema itatoa onyo la mapema kwa mtu mwenye dalili za saratani hiyo.
Sidiria hiyo kwa jina Eva iliotengezwa naye na marafikize watatu walianzisha kampuni hiyo pamoja.
Lakini wamechangisha fedha ili kuifanyia majaribio na wiki hii wakashinda tuzo katika hafla ya wanafunzi wanaotaka kufanya biashara.
Kampuni yao Higia Technologies iliibuka mshindi baada ya kuzishinda kampuni nyengine za biashara kutoka kote duniani ili kushinda dola 20,000 kuzalisha wazo lao.
Uvimbe ulio na saratani unaweza kupandisha vipimo vya joto mwilini.

Rais wa Mexico alimpongeza Julian kwa kushinda tuzo la wanafunzi wafanyibiasharaHaki miliki ya picha

Wazo la sidiria ya Eva ni kwamba ina sensa ambazo inaweza kupima viwango vya joto, kuviweka katika programu na kumuelezea kuhusu mabadiliko yanayomsumbua.
Wanawake wanaohitaji sidiria hiyo watalazimika kuivaa kwa dakika 60 hadi 90 kwa wiki ili kupata vipimo vya sawa.
Hii ni awamu ya kwanza ya dalili za ugonjwa huo.
Tayari sidiria hiyo imefanyiwa majaribio na itafanyiwa vipimo vyengine vya kimatibabu kabla ya wataalam wa ugonjwa wa saratani kuipendekeza kuwa njia ya kugundua saratani.
Anna Perman kutoka kituo cha utafiti cha Uingereza kimeambia BBC : Tunajua kwamba uvimbe huo una mishipa isio ya kawaida ya kupitisha damu na tunajua kwamba kasi ya damu katika mishipa sio thibitisho kwamba mtu anakabliwa na saratani.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.