Manchester United na Manchester City kukutana Marekani
Debi ya kwanza ya Manchester kuchezewa nje ya England huenda ikachezewa nchini Marekani majira yajayo ya joto.
City chini ya Pep Guardiola na United chini ya Jose Mourinho, walipangiwa kukutana mjini Beijing, Uchina Julai mwaka huu.
Hata hivyo, hilo halikufanyika baada ya mvua kubwa kunyesha na kuzuia mchezo huo kufanyika uwanja wa Bird's Nest.
Mchezo huo ulifutiliwa mbali saa sita kabla ya kuanza.
Klabu zote mbili zitakuwa Marekani Julai kujiandaa kwa mwanzo wa msimu wa 2017.
Hakujatolewa maelezo zaidi lakini klabu zote mbili zinatarajiwa kushiriki katika Kombe la Bingwa wa Kimataifa.
No comments