Ads

Tetemeko Italia: Siku rasmi ya kuwaomboleza waathiriwa wa tetemeko la ardhi.........

Mazishi ya kitaifa ya watu kadhaa yatafanyika Jumamosi

Image copyright
Siku ya kitaifa ya maombolezi imeanza nchini Italia, kuwaomboleza waathiriwa wa tetemeko kubwa la ardhi, lilokumba maeneo ya katikati mwa taifa hilo.
Waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi atahudhuria mazishi ya kitaifa ya walioaga dunia katika eneo lililopata pigo kubwa, Arquata.
Hali ya tahadhari imetangazwa katika maeneo yaliyoathirika.
Zaidi ya watu 280 wanaaminika kwamba wameaga dunia.
Takriban watu 400 kwa sasa wanatibiwa hospitalini.
Matumaini ya kupata watu wakiwa hai kwenye vifusi vya majengo yaliyobomolewa yanafifia baada ya siku tatu za uokoaji.
Raia wengi wa Italia waliaga dunia, pamoja na raia kadhaa wa kigeni.
Tetemeko la ardhi liliharibu majengo ya kihistoria.Image copyright
Bendera za taifa hilo zitapeperushwa nusu mlingoti.
Zaidi ya watu 200 waliuwawa katika eneo la Amatrice pekee.
Watu 2,000 wameachwa bila makao.
Tetemeko la ardhi lilikuwa na nguvu ya 6.2 katika vipimo vya Richter, lilitokea mapema jumatano, kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Italia Roma.
Mamia ya tetemeko dogo za ardhi yamekwaza juhudi za uokoaji.



Image copyright

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.